Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Taarifa kwa Umma

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Mhandisi Dkt. John Ndunguru na kuivunja bodi hiyo kuanzia leo tarehe 24 Septemba, 2018.

Mhe. Rais Magufuli amechukua hatua hiyo kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba, 2018 na matukio mbalimbali ya ajali za barabarani hapa nchini yanayosababisha vifo, ulemavu na uharibifu wa mali.

Pamoja na hatua hiyo kamati ya uchunguzi ambayo itatangazwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa baadaye leo, itaendelea na uchunguzi wa ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kama ilivyopangwa.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

24 Septemba, 2018

245 thoughts on “Taarifa kwa Umma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama