Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

SSRA Yawapiga Msasa Wabunge Kuhusu Dhana ya Hifadhi ya Jamii

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Onorius Njole akiongea na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu dhana ya Hifadhi ya Jamii na Umuhimu wake kwa Jamii, ambapo alisema moja ya mafanikio ya mamlaka hiyo imewezesha kuhuisha uwekezaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kutoa Miongozo ya Uwekezaji katika semina iliyofanyika leo Bungeni Mjini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akiongea na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa Semina kuhusu dhana ya Hifadhi ya Jamii na Umuhimu wake kwa Jamii iliyofanyika leo Bungeni Mjini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia Semina kuhusu dhana ya Hifadhi ya Jamii na Umuhimu wake kwa Jamii iliyofanyika leo Bungeni Mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) akiongea wakati wa Semina kwa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu dhana ya Hifadhi ya Jamii na Umuhimu wake kwa Jamii iliyoyolewa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)

 

4 thoughts on “SSRA Yawapiga Msasa Wabunge Kuhusu Dhana ya Hifadhi ya Jamii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama