Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

SSRA Yatoa Mafunzo kwa Washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha Kuhusu Umuhimu wa Kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Mwezeshaji Bibi. Sarah Kibonde Msika –Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano kwa Umma na Uhamasishaji, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), akitoa elimu kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Jamii kwa washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Washiriki wa mafunzo wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji Bibi. Sarah Kibonde Msika (hayupo pichani) wakati akitoa mada kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Jamii kwa wananchi.

Bibi. Agnes Lubuva, Afisa Mahusiano kwa Umma na Uhamasishaji, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), akitoa maelezo kwa wananchi kuhusu kazi na wajibu wa SSRA katika kusimamia Hifadhi ya Jamii nchini.

Muonekano wa Banda la Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), katika Maadhimisho ya Wiki ya Fedha yanayoendelea katikaViwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. (Picha zote na: Thomas Nyindo)

40 thoughts on “SSRA Yatoa Mafunzo kwa Washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha Kuhusu Umuhimu wa Kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama