Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yatoa Takribani Shilingi Bilioni 21  Kuboresha Shule 85 za Kata

Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akikagua moja ya miundombinu ya madarasa katika moja ya ziara zake hivi karibuni mkoani Dodoma

Na Frank Mvungi-MAELEZO, Dodoma.

Serikali imetoa takribani Shilingi Bilioni 21 kwa ajili ya kuboresha shule 85 za Kata hapa nchini ili ziwe na Kidato cha Tano na Sita hali itakayoongeza ubora wa kiwango cha elimu na kuimarishwa kwa miundombinu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Selemani Jafo wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) siku za Jumatatu na Alhamisi.

Akifafanua Waziri Jafo amesema kuwa dhamira ya Serikalini katika kuboresha sekta ya elimu ambapo kila mwezi imekuwa ikitoa takribani Bilioni 23 zinazotumika kugharimia elimu bure hali inayochochea kuongezeka kwa wanafunzi wanaojiunga katika shule za msingi na Sekondari .

“Tumejenga madarasa mengi na vyoo vingi ili kuendana na kasi ya udahili wa wanafunzi na pia tutahakikisha kuwa kuna kuwa na uwiano katika mgawanyo wa walimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Aliongeza kuwa Serikali katika kuboresha huduma za Afya imeshapeleka fedha katika vituo 172 kote nchini ili kuboresha huduma zinazotolewa na pia watumishi katika sekta hiyo wataajiriwa kwa kuzingatia mahitaji kutokana na nafasi zilizoachwa wazi baada ya zoezi la ukaguzi wa vyeti  feki.

Aidha Waziri  Jafo aliwataka Viongozi wote katika Mikoa na Halmashauri kusimamia vizuri miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao ili thamani halisi ya fedha zilizowekezwa ionekane.

“Nawasihi watanzania walipe kodi kwa kuwa fedha zinazotokana na kodi ndizo zinazotumika kutekeleza miradi ya maendeleo na ni matumaini yangu kuwa maelekezo niliyotoa kwa wakurugenzi kuhusu ukusanyaji wa mapato yatazingatiwa na watasimamia kazi hiyo vyema na kubuni vyanzo vipya vya mapato”Alisisitiza Jafo.

Aidha Waziri Jafo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa hadi sasa watumishi zaidi ya 300 wameshachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.

Kwa upande wa sekta ya Viwanda amebainisha kuwa wamejipanga vyema kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kutenga maeneo maalum ya uwekezaji katika Halamashauri na Mikoa.

47 thoughts on “Serikali Yatoa Takribani Shilingi Bilioni 21  Kuboresha Shule 85 za Kata

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama