Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

SERIKALI YATOA FEDHA 100% YA MANUNUZI YA DAWA NCHINI

Na. Immaculate Makilika.

 

Serikali imetoa  asilimia mia moja ya fedha za bajeti ya dawa kwa mwaka  2016/2017  kwa ajili ya manunuzi ya dawa ikiwa ni moja ya mikakati ya kuboresha sekta ya afya nchini.

 

Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO na kurushwa  na kituo cha televisheni cha TBC, Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa,  Laurean Bwanakunu alisema kuwa Serikali inawahakikishia  wananchi kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 zipo  fedha za kutosha ili kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya.

 

“Ikiwa ni  asilimia  81 ya upatikanaji wa dawa  pamoja na vifaa tiba katika maeneo ya mjini na vijijini, ambapo Bohari Kuu ya Dawa inahudumia vituo 5642 nchini kote” alisema Bwanakunu.

 

Pia, Bwanakunu alibainisha kuwa  hivi sasa kumekuwepo na upatikanaji wa dawa muhimu 110 kati ya 135   katika vituo  mbalimbali  vinavyotoa huduma za huduma  za afya.

 

Katika kuboresha huduma za usambazaji wa dawa nchini , Bohari Kuu ya Dawa imefanikiwa kufungua maduka ya dawa 7 katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Geita, Mbeya  na Lindi, ambapo  imeanza kusafirisha dawa kwa kutumia  ndege na treni ili kufikisha dawa kwa wakati katika vituo mbalimbali vya afya nchini.

 

Aidha,  Mikoa na Halmashauri  zimetakiwa  kuwasilisha  maombi yao ya  dawa kwa wakati ili kutatua changamoto ya upungufu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya.

 

 

113 thoughts on “SERIKALI YATOA FEDHA 100% YA MANUNUZI YA DAWA NCHINI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama