Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali ya Tanzania Haitambui Uhalali wa Airtel Afrika Limited

Msajili wa Hazina Bw. Athuman Muttuka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Serikali kutotambua mchakato wa Kampuni ya Bharti Airtel kuuza hisa zake leo jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Uwekezaji toka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Joseph Mwaisembe. (Picha na: Frank Shija)

Msajili wa Hazina Bw. Athuman Muttuka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Serikali kutotambua mchakato wa Kampuni ya Bharti Airtel kuuza hisa zake leo jijini Dodoma.

Na. Gerogina Misama

Serikali ya Jamuhuri ya Muugano waTanzania haitambui mchakato uliotangazwa na Kampuni ya Bharti Airtel wa kukaribisha wanahisa wapya ndani ya Kampuni walioiita kwa jina la Airtel Africa Limited.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka amesema kwamba Kampuni ya Airtel Tanzania Plc inamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Bharti Airtel.

“Maamuzi yoyote ya uuzaji  na uhamishaji hisa au ukaribishaji wa wanahisa wapya ndani ya kampuni zinazoshiriki kwenye ubia wetu ndani ya Airtel Tanzania Plc yanapaswa kushirikisha serikali ya Tanzania,” alisema Mbuttuka.

Aidha, Mbuttuka amesema kwamba wawekezaji wanaodaiwa kununua hisa za kampuni ya Bharti Airtel wajue kuwa umiliki wao kwenye kampuni ya Airtel Tanzania utategemea ridhaa ya Serikali ya Tanzania kupitia kwa Msajili wa Hazina na hatima ya mazungumzo yanayoendelea kati Kampuni ya Bharti Airtel na Serikali yanayouhusu umiliki na uendeshaji wa Kampuni.

Kampuni ya Airtel Africa Ltd ambayo ni kampuni tanzu ya Bharti Airtel iliyosajiliwa London Uingereza ilichapisha taarifa kuwa inakusudia kufanya usajili wa awali katika Soko la Hisa la Kimataifa ikiwa na lengo la kuanza kuuza hisa kwenye soko hilo.

Wawekezaji sita waliojotokeza kununua hisa, baadhi ya kampuni hizo ni pamoja na  Warburg Pincus, Tamasek, Singtel na Soft Bank Group International ambapo kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 1.25 kimewekezwa, kiasi hicho  kinachoweza kuongezeka hadi kufikia dola za Kimarekani bilioni 4.4.

Tayari Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza mazungumzo na  Kampuni ya Bharti Airtel kwa nia ya kupata mwafaka wa uendeshaji na umiliki wa Kampuni ya Airtel Tanzania.

148 thoughts on “Serikali ya Tanzania Haitambui Uhalali wa Airtel Afrika Limited

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama