Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Kuendelea Kushirikiana na Wadau Kupambana na Janga la Ukimwi

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Jumanne Issanga akifungua mkutano wa wadau uliolenga kujadili maboresho yanayopaswa kufanywa ili kuongeza ubora wa namna ya kupambana na janga la Ukimwi hapa nchini hasa kwa kuangalia sheria mbalimbali zinazosimamia suala la ukimwi na pia kuweka mikakati bora itakayowezesha kutolewa kwa huduma bora kwa waathirika waliopo katika makundi maalum Jijini Dodoma kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 3,2018.

Na: Frank Mvungi

Wadau  kutoka katika Taasisi mbalimbali hapa nchini wamekutana Jijini Dodoma kujadili na kuweka mikakati ya pamoja na kupitia sheria mbalimbali zinazosimamia mapambano dhidi ya ukimwi  ili kuongeza tija katika huduma zinazotolewa.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo wa wadau Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi  (TACAIDS) Bw. Jumanne Issanga amesema kuwa dhamira ya mkutano huo ni kupitia sheria mbalimbali zilizopo na ambazo zinasimamia mapambano dhidi ya ukimwi hapa nchini ili kuona mapungufu yaliyopo na kuweka mikakati ya pamoja yakusaidia katika kuongeza mapambano hayo na kuboresha sheria zilizopo.

Sehemu ya mkutano wa wadau uliolenga kujadili maboresho yanayopaswa kufanywa ili kuongeza ubora wa namna ya kupambana na janga la Ukimwi hapa nchini hasa kwa kuangalia mapungufu yaliyopo katika mifumo ya sheria ili kuongeza tija katika mapambano dhidi ya janga la Ukimwi hapa nchini unaofanyika Jijini Dodoma kwa siku mbili.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Jumanne Issanga (kushoto) akisisitiza jambo kwa mwanasheria wa Tume hiyo Bw. Miraji Mambo (kulia) wakati wa mkutano wa wadau unaofanyika Jijini Dodoma.

“Tumekutana na wadau hapa Dodoma kujadili kwa pamoja na kuona namna gani tunakuja na mkakati wa pamoja unaotokana na mkutano huu ili tungeze tija katika huduma zinazotolewa kwa waathirika na hasa walio katika makundi maalum” Alisisitiza Issanga

Akifafanua amesema kuwa maazimio  yatakayotokana na kikao hicho yatasaidia Serikali katika kuhakikisha kuwa janga hili linapigwa vita na kila mtanzania na hivyo kufikiwa kwa malengo ya kutokomeza janga hili.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Tume hiyo Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS)  Bw. Miraji  Mambo amesema kuwa wadau wanaoshiriki katika mkutano huo wanatoka katika Taasisi za Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi,NACOFA,TAMISEMI, Wizara ya Afya na wadau wengine wanaoshiriki katika mapambano dhidi ya Ukimwi hapa nchini.

Mratibu wa Ukimwi Tume ya Taifa ya Ukimwi TACAIDS mkoa wa Tanga Bw. Juma Mbilinyi akiwasilisha mada kuhusu hali ya maambukizi ya virusi vya ukimwi hapa nchini katika makundi mbalimbali hapa nchini.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza ASP Michael Kuga kutoka Jeshi la Magereza mkoa wa Iringa akizungumza wakati wa mkutano wa wadau uliolenga kujadili maboresho yanayopaswa kufanywa ili kuongeza ubora wa namna ya kupambana na janga la Ukimwi hapa nchini na pia kuweka mikakati bora itakayowezesha kutolewa kwa huduma bora kwa waathirika waliopo katika makundi maalum.

Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Bw. Miraji Mambo akizungumza wakati wa mkutano wa wadau uliolenga kujadili maboresho yanayopaswa kufanywa ili kuongeza ubora wa namna ya kupambana na janga la Ukimwi hapa nchini na pia kuweka mikakati bora itakayowezesha kutolewa kwa huduma bora kwa waathirika waliopo katika makundi maalum.

Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Bw. Dismas Teti akichangia mada wakati wa mkutano wa wadau uliolenga kujadili maboresho yanayopaswa kufanywa ili kuongeza ubora wa namna ya kupambana na janga la Ukimwi hapa nchini na pia kuweka mikakati bora itakayowezesha kutolewa kwa huduma bora kwa waathirika waliopo katika makundi maalum. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

“Kwa pamoja kwa muda wa siku mbili tunaamini tutapitia sheria mbalimbali na kuona mapungufu yaliyopo ili tutoe mapendekezo ya namna bora ya kuendeleza mapambano haya dhidi ya janga la Ukimwi na hatimaye kufikiwa kwa malengo”; Alisisitiza Mambo

Aliongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa wadau kukutana na kuangali kwa pamoja namna bora ya kufanya mapambano dhidi ya janga hilo yafanikiwe.

Kwa upande wake Mratibu wa Ukimwi TACAIDS mkoa wa Tanga Bw. Juma Mbilinyi amesema kuwa kuna haja kwa jamii kuongeza mwamko wa kupima na kujua hali ili kuchukua hatua stahiki .

Matokeo   ya tafiti zilizofanyika yanaonesha kuwa kuna haja kwa kila mwanajamii kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya janga la ukimwi.

67 thoughts on “Serikali Kuendelea Kushirikiana na Wadau Kupambana na Janga la Ukimwi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama