Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Kuendelea Kuboresha Mazingira ya Wafanyabiashara Nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa uzinduzi wa Program ya maboresho ya usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP) leo Mjini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua Programu ya maboresho ya usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP) leo Mjini Dodoma. (Picha na Daudi Manongi)

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara ili kuchochea
ukuaji wa uchumi na kuvutia wafanyabiasha wa ndani na nje ya nchi.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo leo mjini
Dodoma wakati akizindua awamu ya tano ya programu ya maboresho ya
usimamizi wa fedha za Umma 2017/18 na 2021/22.

Akifafanua Mhe. Samia amesema kwamba katika kuhakikisha kunakuwepo
na usimamizi mzuri wa fedha za umma, Serikali ya Awamu ya Tano
itahakikisha kuwa wafanyabishara wote wanatumia mfumo wa
kielekroniki kulipa kodi.

Aidha amesema kuwa Serikali itaendelea kupunguza matumizi ya fedha
katika Wizara, Taasisi na Idara zake ili fedha hizo ziweze kutumika katika
kuboresha huduma za jamii.

Naye, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa
programu ya maboresho ya usimamizi wa fedha umeleta mafanikio
makubwa ambapo umeongeza makusanyo na mapato ya Serikali Tanzania
Bara na Visiwani.

“Awamu hii ya Tano ya program ya maboresho ya usimamizi wa fedha za
Umma itaweka nguvu na kuimarisha ofisi za wakaguzi wa mahesabu na
kutambua mapungufu yaliyopo katika ofisi hizo,” alifafanua Dkt. Mpango.

Vile vile katika awamu hii maboresho ya kazi za wakaguzi wa ndani
katika Wizara, Taasisi, Idara pamoja mamlaka ya Serikali za mitaa
nchini.

Maboresho ya programu ya usimamizu wa fedha za Umma ulianza mwaka
1998 ikiwa ni awamu ya kwanza ambayo ilihusisha uthibiti matumizi ya
Serikali na kuchangia kukuza uchumi endelevu. Awamu ya pili ilifanyika
mwaka 2004 – 2008 ambayo ilijikita katika kuboresha usimamizi wa fedha
za umma kwa kutumia viwango vya kimataifa. Awamu ya tatu ilifanyika
mwaka 2008 – 2012 ambayo ilihusisha katika kuhakikisha mbinu na
mifumo iliyowekwa awamu ya kwanza inaoanishwa na kutumika ipasavyo
kuleta matokeo yaliyokusudiwa na awamu ya nne ilikuwa mwaka 2012-
2017 ambayo ilenga katika nidhamu katika usimamizi wa fedha za umma
na kutoa huduma bora kwa Umma ili kuleta maendeleo endelevu.

55 thoughts on “Serikali Kuendelea Kuboresha Mazingira ya Wafanyabiashara Nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama