Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali imelipa Tzs milioni 727. 9 kwa wateja 625 wa Benki ya FBME

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akieleza hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wateja wa iliyokuwa Benki ya FBME wanalipwa haki zao kwa mujibu wa sheria mara baada ya kufungwa kwa Benki hiyo.

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba Bungeni mjini Dodoma mapema leo.

Na Beatrice Lyimo- MAELEZO DODOMA

Serikali imesema mpaka kufikia June mwaka huu jumla Shilingi milioni 727. 9 (727,988,000) zimelipwa kwa wateja 625 walioweka fedha zao katika Benki ya FBME.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji leo mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Viti maalumu Mhe. Rukia Ahmed kuhusu hatma ya wateja walioweka fedha zao katika benki ya FBME.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola akieleza mikakati ya Serikali katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu mapema leo Bungeni mjini Dodoma.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu swali bungeni mapema leo kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi kuhusu mikakati ya Serikali kujenga Kambiza JKT katika maeneo mbalimbali hapa nchini kulingana na mahitaji.

Dkt. kijaji amesema kuwa hatma ya wateja endapo Benki au Taasisi ya Fedha itawekwa chini ya ufilisi imeanishwa katika kifungu namba 39(2) na (3) cha Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

” Malipo hulipwa kutokana na Sheria hivyo kinachofanyika ni utekelezaji wa Sheria na Kanuni zake hivyo Serikali haina mpango wowote wa kumuonea mteja yeyote” ameongeza Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji amefafanua kuwa, hatua ya kwanza ni malipo ya fidia kwa Bima ya Amana ambapo kwa mujibu wa Sheria Mteja mwenye amana katika benki anastahili kulipwa fidia ya Bima ya Amana kiasi kisichozidi shilingi za Kitanzania 1,500,000 kutegemeana na kiasi cha salio la amana yake wakati benki inafungwa.

Mbunge wa Viti maalum Mhe. Amina Mollel Akiuliza swali Bungeni leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu

 

Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma wakifuatilia Mkutano wa 9 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unachoendelea mjini Dodoma.

Pia Dkt. Kijaji ameongeza kuwa, hatua ya pili ni malipo kwa wateja ambao fidia ya Bima ya Aman itakuwa ndogo ikilinganishwa na salio la amana yake wakati benki inafungwa.

Aidha, amesema kuwa malipo hayo hutokana na taratibu za ufilisi ambapo mchakato wake unahusisha kukusanya madeni, fedha inayowekezwa katika taasisi nyingine, na kukuza mali za benki.

96 thoughts on “Serikali imelipa Tzs milioni 727. 9 kwa wateja 625 wa Benki ya FBME

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama