Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

RC Tabora: Madiwani Toeni Elimu Wananchi Waondokane na Kilimo cha Kizamani.

Na: Tiganya Vincent; RS-TABORA

MADIWANI Mkoani Tabora wameombwa kusaidia kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo cha kisasa cha mazao mbalimbali ili waweze  kuongeza uzalishaji ambao utaweka mazingira yanayovutia wawekezaji katika sekta ya viwanda vikiwemo vya mafuta ya alizeti.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya wa Kaliua yalikuwa yakiendeshwa na Chuo cha Serikali za Mitaa –Hombolo.

Alisema kuwa wakulima wanapaswa kuelimishwa juu ya ulimaji wa mazao kwa kuzingatia kanuni za kilimo kinachowaondoa kulima kizamani na kupata mazao hafifu ambayo hayana tija kwao na kwa Halmashauri yao na kuanza kulima mazao mbadala kama vile korosho na alizeti kama njia nyingine ya kujiongeza kipato.

“Waheshimiwa Madiwani tusaidieni kuwaelimisha wakulima kuachana kilimo cha kizamani hakiwasaidia kuwainua kiuchumi…wakati tukiwa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda ni vema wakulima waelimishwe juu ya matumizi ya mbegu bora na pembejeo na kulima kwa wakati” alisema Mwanri.

Aliongeza kuwa jukumu la kiongozi mzuri ni pamoja na kuwaonyesha njia sahihi wakulima ili walime  katika utaratibu unaowapa matokeo mazuri yatakayowasaidia kusonga mbele na kuondokana na umaskini.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora amewasaidia kuwa somo ambapo kutokana na mafunzo yake ataanzisha viongozi wengi wanakwenda kuanzisha mashamba la Dasara kwa ajili ya wakulima waweze kujifunza kutoka kwake.

Alisema kuwa wataonyesha juu ulimaji wa kisasa wa mazao mbalimbali ikiwemo pamba , tumbaku, korosho , alizeti na mazao ya chakula ili Halmashauri hiyo iendele kuvuka  lengo la makusanyo ya ndani na hivyo kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua John Pima alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha Maafisa Ugani wanawafikia wakulima wengi ili wawasaidie kuwaelimisha juu ya kuhakikisha wanaendesha kilimo cha kwa kuzingatia kanuni na taratibu za kila zao.

Alisema kuwa mafanikio ya wakulima ndio pia itakuwa fursa kwa kupata mapato mengi ya ndani na hivyo kuongeza nguvu zaidi katika kuboresha mbalimbali wananchi.

 

One thought on “RC Tabora: Madiwani Toeni Elimu Wananchi Waondokane na Kilimo cha Kizamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama