Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais wa Zanzibar Dk Shein Ahudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad S.A.W Zanzibar.

Makamu wa Rais Mstaaf Dkt Mohammed Gharibi Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati akiwasili katika viwanja vya Maisara kuhuhudhuria sherehe za Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad SAW, yaliofanyika Kitaifa katika viwanja vya Maisara Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Al hajj Ali Mohamed Shein, akisalimia na Mwenyekiti wa Kamati ya Maulid ya Mfungo Sita Zanzibar Sheikh Shirali Champsi alipowasili katika viwanja vya Maisara Zanzibar kuhudhuria katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Al hajj Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaaf Dkt. Mohammed Gharib Bilal alipowasili katika viwanja vya Maisara kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Al Hajj Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali wakiwa wamesimama wakati wakutoa Salamu za kumkaribisha qaswida iliokuwa ikisomwa na Madrasatul E Itiswam ya Chukwani Zanzibar.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa na Wananchi na Viongozi wakisimama wakati wa kutoa salamu ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Alhajj Ali Mohamed Shein alipowasili katika viwanja hivyo kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)

Wanafunzi wa Madrasatul E’itiswam ya Chukwani Zanzibar wakisoma Qwasid ya Salamu ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Al Hajj, Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Maisra Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Alhajj Ali Mohamed Shein, alkisoma ratiba ya hafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na kulia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.(

Kadhi Mkuu wa Zanibar Sheikh Khamis Haji akitowa maelezo kabla ya kuaza kwa hafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Zanzibar.

Baadhi ya waalikwa katika hafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) wakifuatilia hafla hiyo katika viwanja vya Maisara Zanzibar

Baadhi ya Waumin wa Kiislam wakihudhuria Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) katika viwanja vya Maisara Zanzibar.

Ustadh Hamadan Juma Hamdan kutoka magogoni Mkoa wa Mjini Unguja akisoma Quran surah Fat-h aya ya 4 hadi ya 10, kabla ya kuaza kwa hafla hiyo.

Waumini wa Kiislam Zanzibar wakihudhuria kuadhimisha sherehe Tufuku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) katika viwanja vya Maisara Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Alhajj Ali Mohamed Shein, akijumuika katika sherehe tukufu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) katika viwanja vya Maisara Zanzibar.

Wanafunzi wa Madrasatul Insania kutoka roundabout magogoni Mkoa wa Mjini Unguja wakisoma Qaswida ya Yarabbi Swalli wakati wa hafla hiyo ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Zanzibar.

Viongozi wa Serikali na Dini Zanzibar wakihudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya maisara wakiwa wamesimama wakati Qiyam Taala. Ikisomwa Qaswida na Madrasatul Qamaria ya kibanda hatari Zanzibar. (Picha na Ikulu)

 

5 thoughts on “Rais wa Zanzibar Dk Shein Ahudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad S.A.W Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama