Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais wa Zanzibar Dk. Shein Afunguzi Jengo la Mtakimu Mkuu wa Serekali Mazizini Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo Jipya la Mtakwimu Mkuu wa Serekali lililopo mazizini Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kulifungua jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar katika maeneo ya mazizini Zanzibar kulia Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohammed (MBM),Mkurugenzi Mkaazi Banki ya Dunia,Ms. Bella Bird na kushoto Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Dk. Ashatu Kijaji wakishiriki katika kukata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo hilo.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Bi, Mayasa Mahfoudh Mwinyi , akitowa maelezo kwa Rai wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea jengo hilo baada ya kulifungua rasmin leo, ikiwa ni shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipanda mti wa mnazi katika eneo la jengo la Mtakwimu Mkuu wa Serikali baada ya uzinduzi wa jengo hilo huko mzizini Zanzibar

Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya Uzinduzi wa engo Jipya la Mtakwimu Mkuu wa Serikali wakifuatilia hafla hiyo wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ai Mohamed Shein, akihutubia. baada ya uzinduzi huo.

 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Tanzania Dk. Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali mazizini Zanzibar.

 

72 thoughts on “Rais wa Zanzibar Dk. Shein Afunguzi Jengo la Mtakimu Mkuu wa Serekali Mazizini Zanzibar

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama