Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Mhe. Dkt. Magufuli Awasilisha Fomu Zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma kwa ajili ya kuwasilisha Fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Makao makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma kwa Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela katika Makao makuu ya ofisi hizo yaliyopo katika Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliokuwepo katika jengo la Sukari House wakati akitoka katika katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati akitoka katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika jengo la Sukari House jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi walio simama kando ya barabara inayopita mtaa wa Ohio wakati akitoka katika Ofisi za za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam. (Picha na Ikulu)

203 thoughts on “Rais Mhe. Dkt. Magufuli Awasilisha Fomu Zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev e┼čyas─▒ depolama