Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Avitaka Vyombo vya Dola Kuwatafuta Waliohujumu Mradi wa Maji Ntomoko

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi pamoja na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa barabara ya Babati Dodoma yenye urefu wa kilomita 251 uliofanyika leo Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakati wa hafla ya uzinduzi wa Barabara ya Babati Dodoma yenye urefu wa kilomita 251 uliofanyika leo Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amevitaka vyombo vya Dola kuwatafuta  na Kuwafikisha mbele ya  vyombo vya sheria wahusika waliohujumu kiasi cha shilingi bilioni 2 katika mradi wa maji wa Ntomoko ulioko wilayani Kondoa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wilayani Kondoa alipokuwa akifungua barabara ya Dodoma hadi Babati yenye kilomita 251.

“Wahusika watafutwe ili warudishe fedha walizochukua au wahakikishe mradi unakamilika. Ni lazima watu waogope mali ya watu masikini,” alisema Rais Magufuli.

Ameendelea kwa kusema, kama viongozi wanawajibu wa kuchukua hatua hata kama zinauma lakini ni kwa manufaa ya Watanzania milioni 55.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewataka wananchi wa wilaya ya Kondoa kuitunza miundo mbinu ya barabara ambayo ameizindua. Aidha amesema wapo Wananchi ambao wamekuwa wakiondoa alama za barabarani na kwenda kutengenezea tela za ng’ombe au kujengea vyoo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuzindua barabara ya Babati Dodoma yenye urefu wa kilomita 251 uliofanyika leo Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Akinwumi Adesina wakati wa hafla ya uzinduzi wa Barabara ya Babati Dodoma yenye urefu wa kilomita 251 uliofanyika leo Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakati wa hafla ya uzinduzi wa Barabara ya Babati Dodoma yenye urefu wa kilomita 251 uliofanyika leo Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Sehemu ya wananchi wa Kondoa wakiwa wamesimama kando ya barabara hiyo kushuhudia uzinduzi wake uliofanywa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza kuhusu umuhimu wa wananchi kutunza miundo mbinu ya barabara wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara ya Babati Dodoma leo Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akisisitiza jambo wakati akitoa salamu za mkoa huo wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara ya Babati Dodoma leo Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Sehemu ya Viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara ya Babati Dodoma leo Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

( Picha zote na Frank Mvungi-  MAELEZO)

Aidha kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema barabara hiyo ni muhimum kwani inaunganisha mikoa ya Dodoma na Manyara, vile vile inarahisisha usafiri baina ya nchi za Kusini mwa Afrika na Kaskazini.

Vile vile amesema barabara hiyo itakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza utalii,  biashara na viwanda kupitia nchi zinapitiwa na barabara hiyo ambazo ni Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe Zambia, Kenya, Ethiopia, Sudan  Misri na Tanzania yenyewe kupita Tunduma, Mbeya, Iringa, Dodoma, Arusha hadi Namanga.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 251 imegharimu shilingi za Kitanzania bilioni 378.423 fedha ambapo Serikali ya Tanzania imetoa shilingi bilioni 107.654 na fedha zilizobaki zimetolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika na Ubalozi wa Japani hapa nchini.

107 thoughts on “Rais Magufuli Avitaka Vyombo vya Dola Kuwatafuta Waliohujumu Mradi wa Maji Ntomoko

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama