Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Ateua Mwingine na Pia Ateua Wengine 2

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Februari, 2019 amemteua Bw. Hosea Ezekiel Kashimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (Public Service Social Security Fund – PSSSF).

Bw. Kashimba anachukua nafasi ya Bw. Eliud Sanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Kashimba alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wengine 2 kama ifuatavyo;

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Augustine Emmanuel Mbokella kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya TIB (TIB Corporate Bank Limited).

Na pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Latifa Mohammed Khamis kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara za Nje (TANTRADE).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza leo tarehe 19 Februari, 2019.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

19 Februari, 2019

91 thoughts on “Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Ateua Mwingine na Pia Ateua Wengine 2

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama