Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Ashiriki Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea baada ya kuizindua rasmi akiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk, Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019. Anayetoa maelekezo ni Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA wa Mahakama ya Tanzania Bw. Enock Kalege na Kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri Mahakama ya Tanzania Mhe. Eva Nkya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteremka kutoka kwenye gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea baada ya kulizindua rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019

2 thoughts on “Rais Magufuli Ashiriki Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama