Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Dkt. Magufuli Alipowajulia Hali Majeruhi wa Ajali ya Moto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na watoa huduma manesi pamoja na madaktari ambao wanahudumia wagonjwa wa ajali ya moto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewatembelea na kuwapa pole majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ambao wameungua moto katika ajali iliyotokea jana asubuhi Mjini Morogoro baada ya mafuta yaliyokuwa yakimwagika kutoka kwenye lori lililopinduka kulipuka moto. Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 71 mpaka sasa.

Majeruhi 46 wamefikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbi kwa magari ya wagonjwa na helkopta na majeruhi wengine wanaendelea kupatiwa matibabu Mkoani Morogoro.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru na Mkuu wa Kitengo cha Wagonjwa wa Dharura cha hospitali hiyo Dkt. Juma Mfinanga wamemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa wagonjwa 46 waliofikishwa hospitalini hapo ni wale walioungua kwa kiwango kikubwa cha hadi takribani asilimia 100 na kwamba 3 kati yao wamefariki dunia baada ya kufika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na watoa huduma manesi pamoja na madaktari ambao wanahudumia wagonjwa wa ajali ya moto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na watoa huduma manesi pamoja na madaktari ambao wanahudumia wagonjwa wa ajali ya moto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kuwapa pole, Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania kutokuwa wepesi wa kuwahukumu kwa madai walikuwa wakiiba mafuta, kwani baadhi yao walikwenda eneo la tukio kwa lengo la kutoa msaada, wengine walikutwa na moto wakiwa katika maeneo yao ya kazi na wengine walikutwa na moto wakiwa wanasafiri katika magari yao.

Mhe. Rais Magufuli amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Hospitali ya Taifa Muhimbili na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa juhudi kubwa wanazozifanya kutoa matibabu kwa majeruhi hao na ameagiza kuwa gharama za matibabu na huduma nyingine kwa majeruhi hao zitatolewa na Serikali.

“Nawashukuru sana Madaktari na Manesi, wanafanya kazi kubwa sana, kweli wanafanya kazi kubwa sana, nimewaona wagonjwa wanahudumiwa vizuri, lakini kikubwa sisi Watanzania tumtangulize Mungu mbele, tuwaombee hawa wagonjwa, lakini na wale waliotangulia mbele za haki nao tuwaombee, na niwaombe ndugu zangu Watanzania katika ajali tusiwe wepesi wa kuhukumu, nimefika humu wodini nimemkuta mmoja ni dereva wa lori la mafuta, alipofika pale aliamua kushuka aende akasaidie, lakini nae ameungua na amelazwa hapa, yupo mwingine alikuwa anasafiri kwenda Mtwara, wala hakwenda kuchukua mafuta, nae ameungua” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi waliokuwa nje ya wodi ya Kibasila.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea katika wodi ya Kibasila kwa ajili ya kuwajulia hali majeruhi hao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na watoa huduma manesi pamoja na madaktari ambao wanahudumia wagonjwa wa ajali ya moto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuwatangaza majeruhi wote kwa majina yao na mahali wanakotoka ili ndugu na jamaa zao wapate taarifa.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru kumruhusu Bi. Rahel Kitwai Roita mkazi wa Turiani Morogoro kuuchukua mwili wa Marehemu mama yake, baada ya mwili huo kuzuiwa kutokana na kudaiwa zaidi ya shilingi Milioni 5 ambazo ni gharama za matibabu.

Bi. Rahel Kitwai Roita ametoa ombi hilo akiwa pembezoni mwa njia ya kupita wagonjwa ambapo Mhe. Rais Magufuli ametaka deni hilo la shilingi Milioni 5 adaiwe yeye na ametoa rambirambi ya shilingi laki 5.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

11 Agosti, 2019

122 thoughts on “Rais Dkt. Magufuli Alipowajulia Hali Majeruhi wa Ajali ya Moto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama