Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Dkt. Magufuli Afanya Mazungumzo na Mgeni Wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya kupita kwenye Gadi ya Heshma katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Museveni wakati akiangalia kikundi cha ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya siku moja nchini.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na wanahabari hawapo pichani mara baada ya kikao chake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari hawapo pichani mara baada ya kikao chake na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuzungumza na wanahabari leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kutoka kwenye chumba cha mkutano wa Wanahabari leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni mara baada ya mazungumzo yao leo Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ikulu).

218 thoughts on “Rais Dkt. Magufuli Afanya Mazungumzo na Mgeni Wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama