Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Dkt. John Pombe Magufuli Azindua Hospitali ya Taaluma ya MUHAS Kampasi ya Mloganzila

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akielezea ujenzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila wakati wa ufunguzi wa hospitali hiyo mapema hii leo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu akizungumza na wananchi wa Mloganzila wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila mapema hii leo.

Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong akisoma hotuba yake kwa Kiswahili fasaha na baadaye kupongezwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila leo. Hospitali hiyo imejengwa na kampuni kutoka Korea Kusini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mloganzila wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila mapema hii leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila mapema hii leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wakazi wa Mloganzila mara baada ya ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila mapema hii leo.
Picha : MAELEZO

132 thoughts on “Rais Dkt. John Pombe Magufuli Azindua Hospitali ya Taaluma ya MUHAS Kampasi ya Mloganzila

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama