Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Prof. Mbarawa Ataka Wananchi Kunufaika na Uwanja wa Ndege Geita

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimia wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017.Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.

Na: Mwandishi wetu

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewataka wananchi wa mkoa wa Geita kutumia fursa ya ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kisasa wa Geita kujikomboa kiuchumi.

Profesa Mbarawa amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la uwanja huo katika kijiji cha Nyabilezi mkoani Geita na kumsisistiza kila mwananchi kuangalia namna atakavyonufaika na uwanja huo.  


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.

“Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba usafiri wa anga unaimarika ili kurahisisha huduma ya usafirishaji wa abiria, hivyo kuvutia watalii katika vivutio mbalimbali nchini”, amesema Profesa Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa, amewataka wakazi wa Kanda ya Ziwa, kutumia fursa ya uwepo wa Uwanja wa ndege huo kukuza utalii, kilimo, ufugaji na biashara ya madini ili kuhuisha uchumi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Waziri Mbarawa ameongeza kuwa katika kuhakikisha usafiri wa anga nchini unaimarika, Serikali  imekarabati viwanja vya ndege vya Mpanda, Bukoba, Tabora na Mafia na ina mpango wa kuvijenga kwa kiwango cha kisasa viwanja 11 nchini ili kuwezesha ndege mpya za Shirika la Ndege  (ATCL), kutoa huduma katika mikoa mbalimbali.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, amesema ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa mkoa wa Geita ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya usafiri wa anga nchini ya mwaka 2003 inayooelekeza uwepo wa uwanja wa ndege wa kisasa katika kila mkoa ili kurahisisha uchukuzi na kuchochea fursa za kibiashara na kitalii katika maeneo mbalimabali ya nchi.

Mhandisi Mfugale, ameongeza kuwa Uwanja wa ndege wa Geita unajengwa na Mkandarasi wa ndani kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 41.

“Uwanja huu utakapokamilika utawezesha ndege kubwa aina ya Boeing 737 – 800 zenye uwezo wa kubeba abiria 100 hadi 200 kuruka na kutua, hivyo kurahisisha huduma ya usafiri wa anga katika ukanda huu”, amesema Mhandisi Mfugale.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (akifuatiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigalla King, Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Lughumbi) wakipanda mti wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.

Wabunge wa Mkoa wa Geita wakipanda mti wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara na mkoa wakikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo. (Picha na Mpiga Picha Wetu)

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi, amesema Mkoa umejipanga kutumia uwanja wa ndege wa Geita katika kukuza utalii na biashara mkoani humo na kuahidi kuulinda uwanja na kutunza miundombinu yake.

Uwanja wa Ndege wa Geita wenye urefu wa Kilometa 3 na upana wa Meta 45 unatazamiwa kuwa na uwezo wa kuegesha ndege kubwa Tatu kwa wakati mmoja pindi utakapokamilika.

87 thoughts on “Prof. Mbarawa Ataka Wananchi Kunufaika na Uwanja wa Ndege Geita

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama