Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Polisi Tabora Inawashikilia Raia 21 wa DRC kwa Tuhuma za Kuingia Nchini Bila Kufuata Utaratibu.

TIGANYA VINCENT, RS –TABORA

JESHI la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia wahamiaji haramu 21 raia wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) kwa tuhuma za kuingia nchini bila kufuata utaratibu.

Taarifa hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora (RPC) Wilbrod Mutafungwa wakati mkutano na waandishi wa habari Ofisini kwake.

Alisema kuwa watuhumiwa hao wa uhamiaji haramu walikamatwa tarehe 17 mwezi huu wilayani Urambo baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

Kamanda huyo wa Mkoa alisema kuwa baada ya wasamaria wema kutoa taarifa kwa Polisi ndipo waliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao ni wa familia tano tofauti za kutoka DRC.

Alisema kuwa katika orodha hiyo wapo wanaume wawili, wanawake watano na watoto 14 ambao walikamatiwa Urambo baada ya kushuka katika gari la abiria la Saratoga linalofanya safari zake kutoka Kigoma hadi Tabora.

Kamanda Mutafungwa aliongeza kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakitatafuta usafiri wa kwenda Tabora mjini kutoka Urambo na ndipo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata.

Alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na Uhamiaji na vyombo vingine kuwahoji sababu ya kuja nchini bila kufuata taratibu inagwa wao wanadai kuwa walikuja kutafuta Kambi ya Wakimbizi kufuatia machafuko yanayoendelea nchini  mwao.

Kamanda Mutafungwa alisema watuhumiwa kutoka familia ya kwanza ni  Dieudonne Buloze (32), Kigwasa Mariya (20), Medianne Buloze (3) na Alber Buloze(1).

Wengine ni Byamungu Mateus(38), Mulasi Nabunane(33), Busime Mateusi(13), Faida Mateusi(8), Mbamba Mateusi(6), Hadija Mateusi(3) ,Bereke Mateusi(2) na Lebinde Omary(60).

Aliwataja wengine walikamatwa kuwa ni Betie Kasongo(24) , Yoshuwa Ekombe (3) , Yosia Ekombe(miezi 10), Aline Chekanabo (28), Francoise Heva (9), Jistin Faiba (7) , Amida Faiba (6), Kikombe Sumaili(4) na Gulenne(miezi 10).

Mmoja wa wahamiaji haramu hao Dieudonne Buloze alikiri kuwa walikimbia DRC kukimbia mapigano yanayoendelea , wakiwa wanatokea Kivu ambapo wavuka mpaka  kupitia ziwa Tanganyika na kujikuta wako upande wa Tanzania.

Alisema wamekuja Tanzania kutafuta hifadhi ili kuokoa maisha yao kutokana na mapigano yanayoendelea baina ya vikosi vya Serikali na Waasi.

Katika hatua nyingine Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa watoto wawili wa shule ya Ncheli katika Kata ya Sungwizi wilayani Simbo wamefariki dunia baada ya kutumbukia katika kisima kilikuwa hakina uzito.

Alisema kuwa chanzo cha vifo hivyo ni wakati mtoto wa kwanza Mwashi Yohana alipoteleza na kuanguka kisimani wakati akijaribu kutaka kunywa maji na ndipo wa pili ajulikanaye kama Wande Shija alifariki baada ya kutumbukia katika kisima wakati akijaribu kumwokoa mwezie.

Kufuatia vifo hivyo Kamanda Mutafungwa alitoa wito kwa wakazi wote Mkoani hapa kuweka uzio katika visima vyote walivyovichimba wakati wa kiangazi na kuhakikisha wazazi wanawasindikiza watoto wao wakati wa kwenda na kutoka shule hasa kwa wale wa shule za awali.

 

18 thoughts on “Polisi Tabora Inawashikilia Raia 21 wa DRC kwa Tuhuma za Kuingia Nchini Bila Kufuata Utaratibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama