Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mama Samia Amuwakilisha Rais Magufuli Mkutano wa SADC Troika Extra Ordinary

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda kumalizika mjini Luanda Angola.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali ya Usalama katika Kanda, Luanda Angola. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri Mkuu wa Lesotho Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Rais Joseph Kabila, Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation), Mhe. Hage Geingob Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

32 thoughts on “Mama Samia Amuwakilisha Rais Magufuli Mkutano wa SADC Troika Extra Ordinary

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama