Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wafanyabiashara China Wavutiwa na Mazingira ya Uwekezaji Nchini Tanzania

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka mji wa Foshan China na Watazania jana Jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyabiashara 20 kuangalia fursa za uwekezaji nchini kufuatia mafanikio ya Kiwanda cha Good One kinachotengeneza vigae. Kauli mbiu ya semina hiyo ni “Kukuza Tanzania na Usanifu wa Makampuni”

Naibu Katibu wa Serikali ya mji wa Foshan nchini China Bw. Lai Zi Ning akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka mji wa Foshan China na Watanzania yenye kauli mbiu ya “Kukuza Tanzania na Usanifu wa Makampuni” iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni wawakilishi wa Kampuni ya Good One Bi. Winnie Mollel

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza Biashara za Kimataifa la Kamati ya Foshan China (CCPIT Foshan) Bi. DENG Xiangwen akisisitiza jambo kuhusu nia yao ya kuwekeza nchini Tanzania wakati wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka mji wa Foshan China na Watanzania yenye kauli mbiu ya “Kukuza Tanzania na Usanifu wa Makampuni” iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni wawakilishi wa Kampuni ya Good One Bi. Winnie Mollel na Bi. Lillian Wu.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiteta jambo na Naibu Katibu wa Serikali ya Foshan Bw. Lai Zi Ning wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka mji wa Foshan China na Watanzania iliyokuwa na kauli mbiu ya “Kukuza Tanzania na Usanifu wa Makampuni” jana Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akishuhudia utiwaji saini mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza Biashara za Kimataifa la Kamati ya Foshan China (CCPIT Foshan) Bi. DENG Xiangwen na Meneja wa Kampuni ya Bordar Ltd Bw. Wu Yahui jana Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akimkabidhi zawadi ya picha Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza Biashara za Kimataifa la Kamati ya Foshan China (CCPIT Foshan) Bi. DENG Xiangwen wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka mji wa Foshan China na Watanzania iliyokuwa na kauli mbiu ya “Kukuza Tanzania na Usanifu wa Makampuni” jana Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wafanyabiashara kutoka mji wa Foshan China na Watanzania uliokuwa na kauli mbiu ya “Kukuza Tanzania na Usanifu wa Makampuni” wakiwa katika mkutano huo jana Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija

4 thoughts on “Wafanyabiashara China Wavutiwa na Mazingira ya Uwekezaji Nchini Tanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama