Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

NBS Yaadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa Kuwajengea Uelewa Wanafunzi Dodoma Sekondari

Kaimu Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Stambuli Mapunda akizungumza na Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma.

Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bibi. Mariam Katemba akiwasilisha mada kuhusu matokeo ya hali ya maambukizi ya Ukimwi kwa vijana mbele ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma.

Mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Seif Kuchengo akiwasilisha mada kuhusu Sensa mbele ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma.

Mwanafunzi wa Kidato cha Nne, Shule ya Sekondari Dodoma, Bi. Najma Mussa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma.

Mwanafunzi wa Kidato cha Nne, Shule ya Sekondari Dodoma, Hassan Hamis Hassan akiuliza swali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma.

Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Dodoma wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Dodoma wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Dodoma wakiangalia vitabu walipotembelea Maktaba ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na NBS ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija)

20 thoughts on “NBS Yaadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa Kuwajengea Uelewa Wanafunzi Dodoma Sekondari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama