Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

NBS Kuendelea Kuzalisha Takwimu Zenye Ubora

  Meneja wa Takwimu za  Mazingira na Mratibu wa shughuli za Malengo Endelevu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja  akisisitiza jambo wakati akifungua warsha ya wadau wa takwimu leo Jijini Dodoma.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imewahakikishia wadau kuwa  itaendelea kuzalisha takwimu bora zinazoendana na mahitaji ya wakati na zitakazosaidia Serikali katika kupima utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na mpango wa pili wa maendeleo hapa nchini.

Akizungumza wakati akifungua warsha ya wadau wa takwimu  inayofanyika mjini Dodoma, Meneja wa Takwimu za  Mazingira na Mratibu wa shughuli za Malengo Endelevu kutoka NBS Bi. Ruth Minja amesema kuwa Dhamira ya Ofisi hiyo ni kuhakikisha kuwa wanazalisha takwimu zenye ubora kwa kuzingatia mahitaji.

”Takwimu zinatumika kupima utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu  na mpango wa pili wa maendeleo hivyo ni vyema tukawajengea uwezo wadau kutoka katika Majiji na Halmashauri ili  tuweze kufanya tathmini ya utekelezaji wake kwa urahisi”. Alisisitiza Bi Minja.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya wadau wa takwimu wakiwemo kutoka katika halmashauri na majiji hapa nchini, mafunzo hayo yamefanyika jijini Dodoma.

Akifafanua Bi. Minja amesema kuwa lengo namba 11 la maendeleo endelevu ni kuweka miji na makazi ya binadamu kuwa salama na yenye maendeleo endelevu hali iliyochochea kufanyika kwa mafunzo hayo kwa wadau.

Kwa upande wake mshauri mwelekezi kutoka shirika la Umoja wa  Mataifa la Maendeleo  (UNDP) Bw. Ambrose Mugisha amesema kuwa anapongeza utendaji wa pamoja katika kufanya tathmini na utekelezaji wa malengo  ya  maendeleo endelevu.

Aliongeza kuwa nchi zinaowajibu wa kushirikiana katika kupiga vita umasikini kupitia utekelezaji wa malengo  ya  maendeleo endelevu.

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa mazingira (NEMC) Bw. Julius  Edward  amesema kuwa wadau wote wa mazingira wanalo jukumu la kusimamia utekelezaji  wa malengo  ya maendeleo  endelevu.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu imekuwa ikiendesha mafunzo yakuwajengea uwezo wadau katika mbalimbali wa takwimu ili waweze kushiriki kikamilifu katika kutumia takwimu kwa maendeleo endelevu na ustawi wa wananchi.

(Picha zote na Daudi Manongi- MAELEZO)

116 thoughts on “NBS Kuendelea Kuzalisha Takwimu Zenye Ubora

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama