Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Watu wa China Akutana na Jaji Mkuu wa Tanzania

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akimkaribisha Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng pindi alipowasili katika Ofisi ya Jaji Mkuu-Mahakama Kuu Zanzibar.

Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng (katikati) akiongea jambo na Mhe. Jaji Mkuu pindi alipomtembelea Desemba 01, 2017.

Majadiliano yakiendelea; pichani ni baadhi ya Wajumbe walioambatana na Naibu Waziri huyo, mbali na Wajumbe hao pia kuna Wajumbe kutoka Mahakama ya Tanzania na Wizara ya Katiba na Sheria, wa pili kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria-Tanzania.

Naibu Waziri wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Zhao Dacheng akipitia nakala ya Kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2020) alichozawadiwa na Mhe.Jaji Mkuu wa Tanzania.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akichangia jambo katika majadiliano baina yake na Naibu wa Waziri wa Katiba na Sheria wa China.

Mhe. Jaji Mkuu akifurahia zawadi ya picha aliyopatiwa na Mgeni wake.

222 thoughts on “Naibu Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Watu wa China Akutana na Jaji Mkuu wa Tanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama