Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Sima Aongoza Ujumbe wa Tanzania Katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Poland

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akisalimiana na Katibu Mkuu wa World Meteorological Organization, Prof. Petteri Taalas. Naibu Waziri Sima anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 24 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Katowice Poland. Kushoto ni Bw. Freddy Manyika Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchi Dkt. Agnes Kijazi akizungumza na Prof. Petteri Taalas Katibu Mkuu wa World Meteorological Organization, katika moja ya mikutano inayoendelea Nchini Poland. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Prof. Petteri Taalas Katibu Mkuu wa World Meteorological Organization, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchi Dkt. Agnes Kijazi na Bw. Freddy Manyika Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira mara baada ya kukamilika kwa kikao baina yao, Katowice Poland.

161 thoughts on “Naibu Waziri Sima Aongoza Ujumbe wa Tanzania Katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Poland

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama