Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Shonza Afanya Ziara Baraza la Sanaa la Taifa (Basata)

Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akimsikiliza Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (wapili kushoto) alipofanya ziara katika Taasisi hiyo na kukagua ukumbi wa maonyesho ya sanaa leo Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akizungumza na watendaji wa BASATA (hawapo pichani) alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiangalia moja ya batiki zinazotengenezwa na wajasiriamali wa fani za sanaa alipofanya ziara katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na watendaji wa BASATA alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia waliokaa ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza. (Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM)

32 thoughts on “Naibu Waziri Shonza Afanya Ziara Baraza la Sanaa la Taifa (Basata)

Leave a Reply to RobertMor Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama