Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Mpina Akutana na Katibu Mkuu Madola

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akiongea jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, baada ya mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaan Leo.

Na. Evelyn Mkokoi-Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira)

Katibu wa Jumuiya ya madola Mhe. Patricia Scotland  amefanya mazungumzo na Naibu Waziri Ofisi ya Mkamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kuhusu suala zima la hifadhi na usimamizi wa mazingira huku eneo la mabadiliko ya Tabianchi likipewa kipaumbele.

Katika mazungumzo hayo Bi. Scotland alisema kuwa kuna kila sababu ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kuelewa zaidi suala zima la mabadiliko ya tabianchi akieleza kuwa wanasayansi wanasema ifikapo mwaka 2050 dunia inaweza kabisa kuepukana na suala la athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi endapo itawezekana kulifanyia kazi kwa pamoja.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mpina alieleza kuwa Tanzania imeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi katika sekta mbalimbali na jitihada zimefanyika katika kuwezesha jamii kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Alisema Serikali inatekeleza Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi (2012) ambapo sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, nishati zimeandaa na zinatekeleza mpango kazi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao.

 Aidha, Mhe. Mpina alipokumbushwa kuhusu jitihada zake zinazoonekana wazi katika suala zima la utunzaji wa mazingira hususan katika oparasheni zake za viwandani, alisema kuwa  viwanda vingi nchini alivyovipitia havina mifumo ya kisasa ya kutibu majitaka akitolea mfano wa jiji la Dar es Salaam ambapo alisema mfumo wa majitaka katika jiji hilo kwa sasa ni asilimia 13% tuu ndiyo yenye mfumo mzuri na kuongeza kuwa asilimia iliyobakia haijakaa vizuri, jambo ambalo si salama kwa viumbe hai na mazingira.

Awali, akiongea katika mkutano huo, Balozi wa Tanzania nchini Uingerea Mhe. Asharose Migiro alitolea mfano wa athari za mabadiliko ya tabia nchi ni katika maeneo ya ufukwe wa Ocean Road ambayo imelika, alisema wakati umefika sasa kwa Tanzania kuonesha ushirikiano katika suala hili na wananchi kuelewa shughuli za kibinadamu zinazochangia kuongeza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na wajumbe walioshiriki mkutano wa masuala ya hifadhi ya mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.

Alisema Serikali inatekeleza Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi (2012) ambapo sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, nishati zimeandaa na zinatekeleza mpango kazi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao.

 Aidha, Mhe. Mpina alipokumbushwa kuhusu jitihada zake zinazoonekana wazi katika suala zima la utunzaji wa mazingira hususan katika oparasheni zake za viwandani, alisema kuwa  viwanda vingi nchini alivyovipitia havina mifumo ya kisasa ya kutibu majitaka akitolea mfano wa jiji la Dar es Salaam ambapo alisema mfumo wa majitaka katika jiji hilo kwa sasa ni asilimia 13% tuu ndiyo yenye mfumo mzuri na kuongeza kuwa asilimia iliyobakia haijakaa vizuri, jambo ambalo si salama kwa viumbe hai na mazingira.

Awali, akiongea katika mkutano huo, Balozi wa Tanzania nchini Uingerea Mhe. Asharose Migiro alitolea mfano wa athari za mabadiliko ya tabia nchi ni katika maeneo ya ufukwe wa Ocean Road ambayo imelika, alisema wakati umefika sasa kwa Tanzania kuonesha ushirikiano katika suala hili na wananchi kuelewa shughuli za kibinadamu zinazochangia kuongeza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola amefanya mazungumzo hayo leo na Naibu Waziri Mpina na Team ya wataalam baada ya kutembelea kisiwa cha Zanzibar.

17 thoughts on “Naibu Waziri Mpina Akutana na Katibu Mkuu Madola

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama