Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Kwandikwa Akutana na Ujumbe wa Bodi ya AFDB

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akifafanua jambo kwa Ujumbe wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), uliofika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma, leo, kupata taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi inayofadhiliwa na Benki hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Steven Dowd, akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa na viongozi wa Wizara ambao wamekutana katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma, leo, kupata taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi inayofadhiliwa na Benki hiyo.

Ujumbe wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), uliofika katika Ofisi za Wizara ya Ujenzi jijini Dodoma, leo, ukimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa wakati akitoa Taarifa ya miradi mbalimbali ya Ujenzi inayofadhiliwa na Benki hiyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma, leo, kupata taarifa ya miradi mbalimbali ya ujenzi inayofadhiliwa na Benki hiyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) pamoja na viongozi wa Wizara hiyo jijini Dodoma, leo, ambapo Ujumbe wa Bodi ya AfDB ulifika katika Wizara hiyo kupata taarifa ya miradi mbalimbali ya ujenzi inayofadhiliwa na Benki hiyo. Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

One thought on “Kwandikwa Akutana na Ujumbe wa Bodi ya AFDB

  • October 25, 2020 at 8:06 am
    Permalink

    all quite the generic viagra online druggist’s at all times cialis generic Thinks fitting Stories -Spoil Placing Paralysed buy generic viagra ef

    Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama