Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Gekul Amuibua Mbaraka Mwinshekhe Mahafali ya Malya

Adeladius Makwega – Kwimba Mwanza (WHUSM)

Serikali imesema kuwa Watanzania wanahitaji burudani ya muziki  kwani  mara baada ya kujishughulisha  na  shughuli  za maendeleo mchana kutwa  basi jioni ni muda wa kupumzisha miili na akili zao.

Hayo yamesemwa Julai 17, 2021 katika mahafali ya 10 ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ambapo Mheshimiwa Pauline Gekul Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amekuwa mgeni rasmi.

“Watanzania tunapenda muziki iwe dansi, Bongo fleva, rege au muziki wa kiutamadauni, si mmeona wanachuo cha Malya walivyokuwa wakicheza muziki vizuri, huku wakinengua?  huo ndiyo muziki” alisema  Mheshimiwa Gekul.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama