Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Biteko Awataka Wachimbaji wa Jasi Kuungana

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akiwa katika kijiji cha Hotel Tatu katika eneo ambalo Madini ya Jasi yanahifadhiwa kwa muda tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda kwenye viwanda mbalimbali nchini. Wengine katika picha ni Kamishna Msaidizi wa Kanda ya Kusini, Mayigi Makolobela (wa pili kushoto), wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai na wengine katika picha ni watumishi wa madini pamoja na wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo.

Na Rhoda James, Lindi

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka Wachimbaji wa Madini ya Jasi kuungana ili kuweza kuandaa Kanuni ndogo ndogo kwa ajili ya kukabiliana na changamoto katika utekelezaji wa shughuli zao ikiwemo ya Bei ya Madini hayo.

Aliyasema hayo leo wakati alipowatembelea  Wachimbaji Wadogo katika ziara ambayo inalenga kutatua migogoro iliyopo katika sekta husika katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Naibu Waziri alisema kuwa bei ya madini ya Jasi imekuwa ikitofautiana kutokana na kukosekana kwa umoja baina ya wachimbaji wa madini hayo.

“Jiungeni pamoja mpange bei ya kuuza Jasi kwa pamoja na mkiwa kitu kimoja changamoto hizi hazitakuwepo,” amesisitiza Biteko.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akimsikiliza Kamishna Msaidizi wa Kanda ya Kusini, Mayigi Makolobela (kushoto), wakati alipotembelea kijiji cha Hotel Tatu kwa ajili ya kujionea Madini ya Jasi yanayozalishwa na Wachimbaji Wadogo. Wengine ni Watumishi wa Madini pamoja na wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo.

Pia, Naibu Waziri alisema kuwa, ameelezwa kuwa ipo changamoto ya miundombinu ya barabara na hivyo kuitaka Halmashauri ya Kilwa kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo   kwa kuwa  itatumka kwa  shughuli mbalimbali.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mayigi   Makolobela alisema kuwa Jasi inayochimbwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara ina ubora wa asilimia 89-95 na iko juu ukilinganisha na Jasi inayopatikana nchi  jirani.

Vilevile, Makolobela ameeleza kuwa kiwango cha Jasi kilichochimbwa katika kipindi cha Mwezi Julai hadi Desemba, 2017 kilikuwa tani 44,500 na gharama yake ilikuwa Shilingi bilioni 4.6.

Aliongeza kuwa, katika kiasi hicho cha Jasi kilichopatikana Serikali imekusanya Mrabaha wa shilingi milioni 138 kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2017.

Naye Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo wa Jasi Mkoa wa Lindi, Peter Ludvick alimweleza Naibu Waziri kuwa ikiwa Serikali itawasaidia  suala la miundombinu hususan  barabara wachimbaji watazalisha mara tatu ya kiwango wanachokizalisha hivi sasa.

68 thoughts on “Naibu Waziri Biteko Awataka Wachimbaji wa Jasi Kuungana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama