Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mzee Mwinyi Amuombea Dua na Kumjulia Hali Dkt. Kigwangalla

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akimuonesha eneo lenye jeraha Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi (katikati) na kushoto ni Mke wa Mzee Mwinyi, Bi. Siti Mwinyi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi leo Agosti 29,2018 amemtembelea na kumuombea dua maalum Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) akiuguza majeraha ya mkono aliyopata katika ajali iliyotokea Agosti 4, mwaka huu Mkoani Manyara.

Mzee Mwinyi aliambatana na Mkewe ambapo wamemjulia hali pamoja na kufanya dua hiyo ili aweze kupona haraka kurejea kwenye majukumu yake ya kitaifa.

“Nimefika leo kukujulia hali na upokee dua hii upone haraka. Sisi tunaendelea kukuombea muda wote” alieleza Mzee Mwinyi.

Kwa upande wake Dkt. Hamis Kigwangalla amemshukuru Mzee Mwinyi na Mama Mwinyi kufika kumjulia hali ambapo awali alimuelezea kuwa anaendelea vizuri na muda wowote ataruhusiwa.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi akiteta jambo na Dkt Hamisi Kigwangalla alipomtembelea kumjulia hali katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI. Kushoto ni Mke wa Mzee Mwinyi, Bi. Siti Mwinyi

“Nashukuru kufika kwenu na sasa naendelea na mazoezi vizuri huku kubwa nikisubiria ruhusa ya madaktari wanaoendelea kunipatia matibabu” alieleza Dkt. Kigwangalla.

Katika upande wa Dkt. Kigwangalla afya yake imeendelea kuimarika zaidi ambapo Agosti 29 ameweza kutembea umbali wa zaidi ya Kilometa nane  ambapo hii ni hatua nzuri kwani kila siku amekuwa akiongeza umbali wa kutembea kwa lengo la kufanya mazoezi ya viungo vyake.

Dkt. Kigwangalla alihamishiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI tarehe 12/08/2018 baada ya kupata matibabu ya awali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwa sasa bado anaendelea na tiba kuuguza mkono wake wa kushoto.

Na Andrew Chale

136 thoughts on “Mzee Mwinyi Amuombea Dua na Kumjulia Hali Dkt. Kigwangalla

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama