Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mwakyembe Ataka Ubunifu katika Filamu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akieleza mikakati ya Serikali katika kutatua changamoto za wasanii wa filamu nchini wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Na.Paschal Dotto.

Wasanii wa filamu wametakiwa kuongeza ubunifu na ubora katika utengenezaji wa filamu ikiwemo kupanua soko nje ya mipaka ya Tanzania ili kujitangaza zaidi na kujiongezea kipato kama wasanii na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na Wadau wa Filamu nchini, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa katika kujenga Taifa la viwanda tasnia hiyo lazima ibadilishwe na wanaotakiwa kubadilika ni wasanii wenyewe ili kuishawishi Serikali kutoa ushirikiano.

Waziri amesema kuwa katika kujenga mafanikio makubwa katika Sanaa ya filamu lazima mazingira wezeshi yawekwe na kwamba Serikali ipo tayari kuweka Sera inayoendana na ulimwengu wa filamu ili kuweza kutoa mchango mkubwa katika utengenezaji wa filamu.

Baadhi ya wasanii wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipokutana nao ili kujua changamoto zinazo ikabili tasnia ya filamu mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

“Tuboreshe kiwango katika kutengeneza sinema zetu kwa weledi ili tuweze kuwashawishi Watanzania ili kuendana na soko la filamu, ‘’ alisema waziri Mwakyembe

Katika kutetea maslahi ya wasanii hao, Dkt. Mwakyembe amewataka kuhakikisha kuwa mikataba inayofungwa kati ya wasanii na makampuni inakuwa ya wazi na yenye malengo ya kutoa faida kwa pande zote mbili, yaani kati ya msanii na mwajiri wake ama kampuni ili kusiwe na mikanganyiko katika tasnia hiyo.

Aidha, Waziri Mwakyembe amesema Serikali inaunga mkono mabadiliko ya tasnia hii lakini mabdiliko yanahusisha wasanii wenyewe na kwamba watumie ubunifu wao ili kuionesha Serikali nia ya ushirikiano. Ametoa mfano wa kazi nzuri zilizoweza kuchukua tuzo kwa ubora wa kazi hizo ambazo ni T-junction, Kiumeni pamoja na Home coming na kuwaasa kuwa hii ni mifano halisi kwa maisha ya Watanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa filamu nchini mara baada ya kumaliza mkutano wao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Pix 04: Mdau wa filamu nchini Prof. Martin Mhando akielezea changamoto mbalimbali zinazoikumba tasnia hiyo wakati wa mkutano wa wadau wa filamu na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe mapema hii leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Eliphace Marwa).

Kwa upande wa taasisi za fedha zikiwemo CRDB, NMB, KCB, na Standard Chartater Bank zimewashauri wasanii kutengeneza filamu zinazokidhi viwango vya kimataifa ili taasisi hizo za kifedha ziweze kuwaunga mono kwa kutangaza bidhaa za taasisi hizo katika filamu na hivyo kuwaongezea kipato.

Naye Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo amesema kuwa Bodi hiyo imeweza kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu kwa kusajili makampuni mbalimbali ya usambazaji wa filamu Tanzania na kwamba kuna zaidi ya makampuni 250 ya usambazaji wa filamu, majumba saba ya sinema, vibanda 30,000 vya kuoneshea sinema pamoja na kuonezeka kwa tuzo kutoka tuzo tisa hadi tuzo 73.

Bi. Fisoo amsema tasnia ya filamu ni mwanzo mzuri wa kutangaza utalii wa nchi kwa hiyo wasanii katika nchi hii wanapaswa kuwa wabunifu katika kufanya kazi zao kwa kuchagu sehemu maalumu za kiugizia hususani katika sehemu za vivutio vya utalii.

Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzanuia Bw.Simon Mwakifamba ameishauri Serikali kujenga eneo maalumu kwa ajiri ya uigizaji wa filamu na kulitumia kama kituo maalumu kwa kutengeneza sinema zao kwa ubunifu wa hali ya juu ikiwemo kutumia tasnia ya filamu kutangaza utalii

 

 

 

 

90 thoughts on “Mwakyembe Ataka Ubunifu katika Filamu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama