Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mkuu wa Soko Kuu Arusha Mbaroni kwa Ubadhirifu

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni (wa kwanza kushoto) akishuhudia ukaguzi wa daftari analotumia Mkuu wa soko kurekodi taarifa za wafanyabiashara jiji la Arusha, wakati wa muendelezo wa operesheni ya ukusanyaji wa mapato.

 

Mfanyabiashara wa Soko Kuu Bw. Daniel Mushi (kushoto) na Mkuu wa Soko kuu la Jiji la Arusha Bw. John Ruzga wakati walipowekwa chini ya ulinzi katika operesheni hiyo ya ukusanyaji wa mapato.

Na Fatuma S. Ibrahimu – Arusha Jiji

Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni ameamuru Mkuu wa soko kuu la Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw. John Ruzga kuwekwa chini ya ulinzi baada ya  kubainika kupokea fedha za wafanyabiashara kwa kigezo cha kwenda kuwalipia ushuru na kutozifikisha Halmashauri kitendo ambacho ni kinyume cha utaratibu wa Serikali mtumishi wa umma.

 “Kitendo alichokifanya mkuu wa soko cha kukusanya fedha za wafanyabiashara kwa kisingizio cha kuwalipia ushuru ni kinyume na sheria na ameinyima mapato serikali hivyo naamuru awekwe chini ya ulinzi akatoe maelezo ya kina juu ya suala hili” Alisema Dkt. Madeni.

Naye Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw. Baltazar Ngowi amwataka wafanyabiashara katika soko hilo kudai risiti pindi wanapolipa ushuru wa vibanda.

“Kutoa pesa bila kudai risiti pia ni kosa kisheria hivyo nichukue fursa hii kuwakumbusha wafanyabiashara  mdai risiti pindi mnapolipa ushuru wa vibanda vyenu na mnapaswa kupeleka fedha zenu wenyewe badala ya kutuma mtu ili kuepuka kadhia ya kutapeliwa ” Alisema Bw. Ngowi

Dkt. Madeni yupo katika wa muendelezo wa operesheni maalum ya ukusanyaji wa mapato ikiwa na lengo la kuongeza mapato ya serikali na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali, pia kuhakikisha wafanyabiashara wote na wamiliki wa vibanda wana leseni za muda husika, risiti halali za kodi  na mikataba halali ya Halmashauri.

159 thoughts on “Mkuu wa Soko Kuu Arusha Mbaroni kwa Ubadhirifu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama