Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP Phaustine Kasike Aanza Ziara ya Kikazi Mkoani Iringa

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Hassan Mkwanda na Maafisa wengine wa Magereza Mkoani Iringa, muda mfupi alipowasili leo Novemba 8, 2018 Mkoani humo. CGP Kasike yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua magereza yote ya Mkoa wa Iringa na kuzungumza na Maafisa na askari pamoja na kujua chamgamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Mhe. Richard Kasesela akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike walipokutana Mkoani Iringa alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi, leo Novemba 8, 2018.

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Iringa wakisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike walipokutana Mkoani Iringa alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Hassan Mkwanda akimkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(katikati meza kuu) ili azungumze na baadhi ya Maafisa na askari wa Gereza Iringa(hawapo pichani, leo Novemba 8, 2018 . Kulia ni ACP. Josephine Semwenda ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi.

Baadhi ya Askari wa Gereza la Wilaya Iringa wakifuatilia maelekezo katika Baraza lililoongozwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ambapo askari hao wameelezea changamoto zao kiutendaji leo Novemba 8, 2018.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Mhe. Richard Kasesela(watatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa tatu toka kulia) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Iringa ( Picha na Jeshi la Magereza).

21 thoughts on “Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP Phaustine Kasike Aanza Ziara ya Kikazi Mkoani Iringa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama