Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

MKURABITA Yaleta Neema Kwa Wananchi Morogoro

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania  (MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe akieleza mafanikio ya Mpango huo katika Mkoa wa Morogoro ikiwemo kuwezesha wananchi kurasimisha ardhi na kupatiwa hati  za kumiliki maeneo yao. kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Ernest Mkongo  leo mjini Morogoro walipomtembelea Ofisini kwake.

Na; Frank Mvungi

Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara  za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmashuri ya Manispaa ya Morogoro wamefanikisha upimaji wa viwanja  1,080 katika manispaa hiyo.

Akizungumza  na Wakazi wa Kata ya Kihonda mjini Morogoro Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania  (MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuwezesha wananchi kujiletea maendeleo kupitia mpango huo wa urasimishji.

“ Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwawezesha wananchi imeanzisha dirisha moja la huduma kwa wananchi katika manispaa ya Morogoro ili kurahisha upatikanaji wa huduma za uwezeshaji kwa wananchi ili waondokane na umasikini” Alisisitiza Bi. Mgembe.

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania  (MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe akisisitiza umuhimu  wananchi wa Kata ya Kohonda  kutumia hati za ardhi walizopata baada ya kurasimisha ardhi ili kuchochea maendeleo katika maeneo yao.

Akifafanua amesema kuwa wananchi waliokwisha nufaika na urasimishaji  wa ardhi kupitia mpango huo  watumie hati za umiliki wa ardhi kujiletea maendeleo ikiwemo kujipatia mikopo kwenye Taasisi za Fedha.

Pia aliwataka wananchi ambao wameshapimiwa maeneo yao kupitia mpango huo wa urasimishaji kwenda kuchukua hati zao katika Mamlaka husika ili wazitumie katika kuchochea maendeleo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishji Bw. Japhet Werema alibainisha kuwa Mpango huo unazijengea uwezo Halmashuri ili ziweze kushiriki katika urasimishaji wa ardhi mijini na vijijini.

Aliongeza kuwa mpango huo unawahamasisha wananchi kutumia ardhi kama nyezo muhimu katika kujiletea maendeleo na kuwataka wananchi kujitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali kukuza uchumi kwa kujenga uchumi jumuishi.

Kaimu  Mkurugenzi wa Urasimishaji Bw. Japhet Werema akieleza mafanikio ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania  (MKURABITA) katika mkoa wa Morogoro leo  walipowatembelea wanufaika wa mpango huo katika Kata ya Kihonda .

Katika taarifa yake mpima ardhi wa Halmashuri ya Manispaa ya Morogoro Bw. Saimon Seja amesema kuwa Viwanja 558 katika mtaa wa Tuelewane vimepimwa, 264 Mtaa wa Kihonda B, Folcal Land 258 hivyo kufanya jumla ya viwanja 1080.

Aliwaasa wananchi walionufaika katika mpango wa urasimishaji kufika katika manispaa hiyo kuchukua hati  za umiliki wa viwanja vyao.

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli imekuwa ikisisitiza ujenzi wa uchumi shirikishi, katika kutekeleza azma hiyo  MKURABITA imekuwa ikionesha mfano katika kuwawezesha wananchi kushiriki kwa vitendo katika ujenzi wa uchumi huo.

 

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania  (MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe akisisitiza umuhimu wa hati za ardhi kwa wananchi wa Kata ya Kihonda mjini Morogoro leo wakati alipotembelea eneo hilo kujinea jinsi wananchi wanavyoendelea kunufaika na mpango huo.

Sehemu ya wananchi wa Kata ya Kihonda mjini Morogoro wakimsikiliza Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania  (MKURABITA)  Bi. Seraphia Mgembe (hayupo pichani) wakati alipowatembelea kuona namna wanavyoendelea kunufaika na fursa zinazotokana na urasimishaji wa ardhi katika eneo hilo.

Afisa Mtendaji wa mtaa wa Kihonda A Bi. Asha Sechonge (kulia) akimkabidhi  Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania  (MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe ripoti ya utekelezaji wa kazi za mpango huo katika eneo hilo ikiwemo upimaji wa viwanja na utoaji wa hati.

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania  (MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kata ya Kihonda mjini Morogoro leo wakati walipotembelea eneo hilo kujinea jinsi wananchi wanavyoendelea kunufaika na mpango huo.

Kaimu  Mkurugenzi wa Urasimishaji Bw. Japhet Werema akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kata ya Kihonda wakati wa ziara ya Mratibu wa Mpango huo kujinea jinsi wananchi wanavyotumia fursa  ya urasimishaji wa ardhi kujiletea maendeleo.

Mpima  ardhi  wa Halmashuri ya Manispaa ya Morogoro Bw. Saimon Seja akitoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazopaswa kufuatwa na wananchi ili kupatiwa ardhi mara baada ya kurasimishiwa ardhi zao katika mkoa wa Morogoro.

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania  (MKURABITA) Bi.Seraphia Mgembe akihamasisha wananchi kushiriki kikamilifu kujiletea maendeleo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kuwawezesha.

 (Picha zote na Frank Mvungi)

25 thoughts on “MKURABITA Yaleta Neema Kwa Wananchi Morogoro

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama