Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Milioni 500 zatumika kuleta neema ya maji Charambe na Kibondemaji

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wakati wa kukabidhi miradi ya maji ya Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha huduma hiyo kwa wananchi.

Na; Mwandishi wetu

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameikabidhi DAWASA miradi miwili ya majisafi na usafi wa mazingira yenye thamani ya milioni 500 na inahudumia wananchi wasiopungua 160,133 lengo likiwa kuwafikia wananchi 280,000 katika Wilaya ya Temeke.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa, Naibu Waziri Mhe. Aweso amesema kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuimarisha huduma za maji katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mbalimbali hapa nchini ili kufikia malengo yaliyowekwa kufikia mwaka 2020.

“Mradi  huu wa majisafi una uwezo wa kuzalisha lita laki 224,000 za maji kwa siku na utahudumia wakazi wa Charambe na Kibonde maji katika Manispaa ya Temeke ambapo wananchi wameanza kuunganishiwa huduma hii ya maji kupitia  Ofisi ya DAWASA  Temeke”. Alisisitiza Mhe.  Aweso

Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi miradi ya maji ya Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha huduma hiyo kwa wananchi.

Kuanza kwa mradi huu kunasaidia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo hayo na kuchangia  katika kukuza shughuli za uzalishaji na maenedeo katika maeneo hayo.

Kwa upande wa mradi wa kuchakata  majitaka Mhe. Aweso amebainisha kuwa mradi huo una uwezo wa kuchakata lita 50,000 za majitaka kwa siku ambapo mradi huo utasaidia upatikanaji  wa mbolea,  maji kwa ajili ya umwagiliaji, pamoja na gesi.

DAWASA imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika  kuimarisha huduma zake ikiwemo kudhibiti uvujaji wa maji na kuweka mtandao mpya katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya majisafi na salama.

 

 

 

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akikata utepe kuzindua miradi ya maji Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya washiriki wa hafla ya kukabidhi miradi ya maji ya Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha huduma hiyo kwa wananchi.

85 thoughts on “Milioni 500 zatumika kuleta neema ya maji Charambe na Kibondemaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama