Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mhandisi Masauni atembelea Mradi wa Maji Kikwajuni-Zanzibar.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (wa tatu kushoto) akiongea na Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kushoto) alipotembelea Mradi wa Maji wa Kikwajuni, uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein miaka miwili iliyopita ikiwa ni juhudi za Mbunge huyo kushirikisha wadau katika kuhudumia na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Jimbo hilo. Kuilia ni Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mhandisi Mohamed Elyas na anayefuata ni Katibu wa Taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Icon (TAYI), Abdallah Ahmed Suleiman.

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mhandisi Mohamed Elyas wakati wakiondoka baada ya kumuongoza Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kushoto), kutembelea Mradi wa Maji wa Kikwajuni ikiwa ni sehemu ya kushirikiana na wadau kuhakikisha tatizo la upungufu wa maji linamalizika katika jimbo la Kikwajuni. (Picha na Abubakar Akida)

(Picha na Abubakar Akida)

 

 

19 thoughts on “Mhandisi Masauni atembelea Mradi wa Maji Kikwajuni-Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama