Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mfumuko wa Bei Wazidi Kupungua

Na. Thobias Robert- MAELEZO.
Mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na sizizo za vyakula umepungua kwa mwezi Agosti kwa
asilimia 5 ikilinganishwa na mwezi Julai ambao ulikuwa ni asimilia 5.2, huku Fahirisi za bei
zikipungua hadi 108.46 ikilinganishwa na mwezi Julai ambayo ilikuwa ni 108.85.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii
Bw. Ephraim Kwesigabo katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ofisi ya Taifa ya
Takwimu ikiwa ni lengo la ofisi hiyo kuujulisha umma juu ya mfumuko wa bei kwa bidhaa za
vyakula na nishati hapa nchini.

“Kupungua kwa Fahirisi za bei kwa mwezi Agosti kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za
baadhi ya vyakula hapa nchini pamoja na baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kama vile Dizeli
pamoja na Petroli,” alifafanua Bw. Kwesigabo.

Aidha Bw. Kwesigabo, alivitaja baadhi ya Vyakula vilivyoshuka bei kwa mwezi Agosti ni
pamoja na Mchele kwa asilimia 1.2, mahindi 1.2, unga wa mahindi 1.6, dagaa 3.4, mbogamboga
1.2, maharage 3.2 viazi 3.5, pamoja na ndizi za kupika 2.4.

Vilevile Bw. Kwesigabo alizitaja baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kushuka kwa
mfumuko wa bei kuwa ni Dizeli kwa asilimia 2.2, Petroli asilimia 2.4 pamoja na vifaa vya
kielektroniki kwa asimilia 1.6. lakini pia aliongeza kuwa mfumuko wa bei kwa kipimo cha
mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani umepungua kwa mwezi Agosti hadi
asilimia 9.1 kutoka asilimia 9.3 kwa mwezi Julai.

Bw. Kwisegabo alisema kuwa thamani ya Shilingi 100 ya Tanzania imeongezeka ikilinganishwa
na mwezi uliopita ambapo alisema, “uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa
na huduma umefikia shilingi 92.20 mwezi Agosti, ikilinganishwa na Shilingi 91.87 ilivyokuwa
mwezi Julai ya mwaka huu.”

Mkurugenzi huyo wa Sensa na Takwimu za Jamii alibainisha kuwa, mfumuko huo umepungua
zaidi ikilinganishwa na nchi ya Kenya, ambapo mfumuko huo umeongeza kwa asilimia 8.04
ikilinganishwa na mwezi Julai ambao ulikuwa asilimia 7.47, kwa upande wa Uganda mfumuko
wa bei umepungua sawa na Tanzania ikiwa ni asilimia 5 ikilinganishwa na 5.2 kwa mwezi Julai.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupitia idara yake ya Sensa na Takwimu za Jamii imekuwa na
utaratibu wa kutoa takwimu za mwenendo wa bei za vitu mbalimbali hapa nchini kila mwisho
wa mwezi ili kuwafahamisha watanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama