Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mechi ya Yanga na Namungo, Uwanja wa Majaliwa Ruangwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wapenzi wa mpira wa miguu baada ya kukagua timu za Yanga na Namungo zilizocheza mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Novemba 18, 2018. Kulia kwake ni mkewe Mary , wapili kushoto ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Timu hizo zilitoka sare 1-1.

Reliant Lusajo wa Namungo FC (kushoto) akimiliki mpira huku akizongwa na Juma Abdul wa Yanga katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Novemba 18, 2018. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare 1-1.

Mshambuliaji wa Yanga, Maka Edward (kulia) akipiga mpira huku akizuiwa na beki wa Namungo, Hashim Manyanya katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Novemba 18, 2018. Timu hizo zilitoka sare 1-1.

Kiungo na mshambuliaji wa Yanga, Thaban Kamusoko akijaribu kufunga kwa tikitaka bila mafanikio mbele ya beki wa Namungo FC, Juma Jamal akimkabili katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Novemba 18, 2018. Kushoto ni Kipa wa Namungo FC, Adam Oseja

Andrew Vincent wa Yanga akizuia mpira kwa kichwa huku akizongwa na Reliant Lusajo wa Namungo katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwa Novemba 18, 2018. Timu hizo zilitoka sare 1 – 1.

Deus Kaseke wa Yanga akimili mpira katika mechi ya kirafiki kati ya timu yake na Namungo iliyochezwa kwenye uwanja wa Majaliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Novemba 18, 2018. Timu hizo zilitoka sare 1 – 1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

134 thoughts on “Mechi ya Yanga na Namungo, Uwanja wa Majaliwa Ruangwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama