Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio ya Bunge katika Picha

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiwasilisha muswaada wa marekebisho ya sheria mbalimbali 13 (Na 2) wa mwaka 2018 (The Written Laws Miscellaneous Amendments) (No.2), Bill,2018 leo Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuondoa changamoto zilizopo katika sekta ya sukari hapa nchini ili kuwalinda wananchi na kuhakikisha kuwa biashara ya sukari inafanyika kwa kuzingatia sheria na kanuni.

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa Kampuni za Madini zinatekeleza dhana ya kutoa huduma za jamii katika maeneo wanayochimba madini ikiwa ni matakwa ya kisheria.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza kuwa Serikali imejenga uwezo katika kuinua sekta ya afya nchini ikiwemo kuongeza bajeti ya dawa na upatikanaji wake katika maeneo ya kutolea huduma yamefikia zaidi ya asilimia 90.

33 thoughts on “Matukio ya Bunge katika Picha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama