Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Ziara ya Waziri Mhagama Ofisi za PSSSF na NSSF Moshi

Baadhi ya wastaafu wakijaza fomu za taarifa zao wakati wa zoezi la uhakiki katika ofisi za PSSSF Moshi mkoani Kilimanjaro Januari 10, 2019

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na baadhi ya wastaafu wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kwa mifuko ya NSSF na PSSSF.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya jamii NSSF Bw.William Erio (katikati) akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama wakati wa ziara yake katika Ofisi za NSSF Moshi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (wan ne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali pamoja na wale wa mifuko ya Hifadhi wakati wa ziara yake katika ofisi za Moshi mkoani Kilimanjaro. Kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya jamii NSSF Bw.William Erio

129 thoughts on “Matukio Katika Picha Ziara ya Waziri Mhagama Ofisi za PSSSF na NSSF Moshi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama