Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha, Ziara ya Rais Magufuli Mkoani Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana naViongozi wa Dini mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ngoma za asili kutoka kikundi cha Bujora mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa sala na viongozi mbalimbali wa dini kutoka Kanda ya ziwa mara baada ya kuwasili mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Kona ya bwiru katika barabara ya Airport wakati akitokea uwanja wa ndege waMwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.

Rais waJamhuri yaMuungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza wakati akielekea Uwanja wa Nyamagana kuangalia mechi kati ya Buhongwa United naTimu ya Nyamwaga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mashabiki waliohudhuria mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mpira pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela katika uwanja wa Nyamagana ambapo timu ya Buhongwa United ilikuwa ikicheza na Nyamwaga FC.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wachezaji wa Buhongwa Fc mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Nyamagana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mashabiki wa mpira wa miguu wakati akitoka katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. (Picha na: Ikulu)

69 thoughts on “Matukio Katika Picha, Ziara ya Rais Magufuli Mkoani Mwanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama