Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Ziara ya Dkt. Abbasi,TAGCO Mkoani Kilimanjaro

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbassi akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro Michael Mwandezi wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea ufanisi na utendaji kazi wa vitengo vya Habari na Mawasiliano katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro jana Ijumaa Mei 25, 2018. Ziara hiyo iliratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kushirikiana na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO).

Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro Michael Mwandezi akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (wa kwanza kushoto) pamoja na wajumbe wa kamati tendaji ya Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) waliotembelea kujionea utendaji kazi wa kitendo cha Habari na Mawasiliano Serikali katika Halmashauri hiyo jana Ijumaa Mei 25, 2018.

Katibu Mkuu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Abdul Njaidi akizungumza jambo wakati wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea ufanisi na utendaji kazi wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mikoani Kilimanjaro jana Ijumaa Mei 25, 2018. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Michael Mwandezi. Ziara hiyo iliratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kushirikiana na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO).

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Michael Mwandezi (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) na wajumbe wa kamati tendaji ya Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) wakiongozwa na Katibu Mkuu, Abdul Njaidi (mwenye koti jeupe) wakati wa ziara yao ya kutembelea na kujionea utendaji kazi wa kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Halmashauri ya Manispaa hiyo jana Ijumaa Mei 25, 2018.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Michael Mwandezi (kushoto) wakati wa ziara ya kutembelea Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini katika Manispaa hiyo iliyofanyika jana Ijumaa Mei 25, 2018 baina yake na wajumbe wa kamati tendaji ya Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO).

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza katika mahojiano ya kipindi maalum cha Redio, Redio Sauti ya Injili iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro jana Mei 25, 2018 kueleza kuhusu utekelezaji wa sera, mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali ya Awamu ya Tano. Katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Abdul Njaidi .

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Magreth John (katikati) akizungumza wakati wa kikao baina yake na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (wa kwanza kushoto) pamoja na wajumbe wa kamati tendaji ya Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kilichofanyika jana Ijumaa Mei 25, 2018 kujionea utendaji kazi wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini katika Halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, Magreth John (wa tatu kulia) na wajumbe wa kamati tendaji ya Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO), mara baada ya kumaliza kwa mkutano baina yao jana Ijumaa Mei 25, 2018.

(NA MPIGAPICHA WETU) 

96 thoughts on “Matukio Katika Picha Ziara ya Dkt. Abbasi,TAGCO Mkoani Kilimanjaro

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama