Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Ujenzi wa Mji wa Serikali leo Januari 1, 2019

atibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma leo wakati wa ziara yakukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe akionesha kazi ya usimikaji wa miundombinu ya umeme inayofanywa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) Dkt. Maulid Banyani akisisitiza jambo kwa Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe wakati wa ziara ya kukagua hatua iliyofikiwa katika majengo ya Wizara yanayojengwa na Shirika hilo katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma ikiwemo la Wizara ya Fedha na Mipango.

Muonekano wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma kama linavyoonekana ambapo ujenzi wake unatarajia kukamilika katika muda uliopangwa.

185 thoughts on “Matukio Katika Picha Ujenzi wa Mji wa Serikali leo Januari 1, 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama