Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Ujenzi wa Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma

Katibu wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kutaribu mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora , jengo hilo linajengwa katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

Sehemu ya mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi katika jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linaloendelea kujengwa katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma kama walivyokutwa mwishoni mwa wiki.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kutaribu mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati linalojengwa katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

Hatua iliyofikiwa katika jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kama inavyoonekana katika picha kwenye mji wa Serikali Ihumwa ambapo ujenzi unaendelea, hayo yamejiri mwishoni mwa wiki wakati Katibu wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kutaribu mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe (hayupo pichani) na ujumbe wake walipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo.

Muonekano wa jengo la Wizara ya Katiba na Sheria katika mji wa Serikali Ihumwa ambapo ujenzi wa majengo ya Wizara zote unaendelea.

Muonekano wa jengo la Wizara ya Maji katika mji wa Serikali ambapo ujenzi wake unaendelea kama ilivyokutwa mwishoni mwa wiki.

(Picha zote na Frank Mvungi)

3 thoughts on “Matukio Katika Picha Ujenzi wa Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama