Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha; Tamasha la Wanawake Wajasiriamali Jijini Dodoma

 

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akisisitiza kuhusu hatua iliyochukuliwa na Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo kupata alama ya ubora wa bidhaa wanazozalisha ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa Viwanda ambapo Serikali inalipa gharama hizo kwa wajasiriamali wadogo, hayo ilikuwa wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.

Afisa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati Bw. Sileja Lushibika akieleza hatua zinazopaswa kufuatwa na mjasirimali ili kupata alama ya ubora kwa mmoja wa wananchi waliofika katika Banda la Shirika hilo wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.

Afisa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Paulus Oluochi akizungumzia umuhimu wa kuzingatia vipimo kwa wajasirimali wakati wa kufungasha na kuzalisha bidhaa mbalimbali ili kuchochea dhana ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda,hiyo ilikuwa wakati wa Tamasha la Mwanamke Mjasiriamali linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchini Burundi.

Afisa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Paulus Oluochi akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa katika kuhakikisha kuwa wajasiriamali wote wanafikiwa na huduma za Wakala huo ili kutekeleza kwa vitendo matwakwa ya sheria ya vipimo na kanuni zake.

Afisa Vipimo wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Bi. Zaidat Gharibu akionesha jinsi wanavyohakiki vipimo mbalimbali ikiwemo upimaji wa gesi yakupikia majumbani.

(Picha zote na Frank  Mvungi)

114 thoughts on “Matukio Katika Picha; Tamasha la Wanawake Wajasiriamali Jijini Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama