Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Semina Kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (aliyesimama), akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na Wizara kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu masuala ya umeme, mafuta na gesi, jana Septemba 8, 2018 jijini Dodoma. Wengine pichani (Meza Kuu) kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Mwenyekiti wa Kamati Dustan Kitandula na Katibu wa Kamati Felister Mgonja.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula (wa pili-kushoto), akifungua semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa wabunge wa Kamati hiyo kuhusu masuala ya umeme, mafuta na gesi, jana Septemba 8, 2018 jijini Dodoma, Wengine kutoka kushoto ni Katibu wa Kamati Felista Mgonja, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Hamisi Mwinyimvua.

Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Hamisi Mwinyimvua, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa wabunge wa Kamati hiyo kuhusu masuala ya umeme, mafuta na gesi, jana Septemba 8, 2018 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamisi Mwinyimvua (aliyesimama) akizungumza, wakati wa semina iliyoandaliwa na Wizara kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu masuala ya umeme, mafuta na gesi, jana Septemba 8, 2018 jijini Dodoma. Wengine pichani kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Kamati Dustan Kitandula na Katibu wa Kamati Felister Mgonja

Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi Raphael Nombo akijisajili kabla ya kuanza kwa semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu masuala ya umeme, mafuta na gesi, jana Septemba 8, 2018 jijini Dodoma.

Sehemu ya wabunge, viongozi na maafisa wa Serikali, wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu masuala ya umeme, mafuta na gesi, jana Septemba 8, 2018 jijini Dodoma.

 (Picha zote na Veronica Simba- Wizara ya Nishati)

 

 

68 thoughts on “Matukio Katika Picha Semina Kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama