Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha; Ofisi ya Waziri Mkuu Wapokea Vifaa vya Ofisi Kuhitimisha Zoezi la Kuhamia Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi. Maimuna Tarishi akisisitiza jambo wakati akipokea sehemu ya vifaa vya Ofisi hiyo vilivyowasili kutoka Jijini Dar es Salaam mapema leo wakati wa hafla fupi iliyofanyika Jijini Dodoma katika Ofisi ya Waziri mkuu.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi. Maimuna Tarishi (kushoto) akieleza jambo kwa sehemu ya watumishi wa Ofisi hiyo pamoja na wajumbe wa kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma leo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya Ofisi hiyo vilivyowasili kutoka Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya vifaa vya Ofisi ya Waziri Mkuu kama vinavyoonekana katika picha mara baada yakufikishwa Jijini Dodoma na gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vikitokea Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Nigel Msangi akionesha sehemu ya vifaa vya Ofisi hiyo vilivyowasili Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha zoezi la Ofisi hiyo kuhamia Dodoma.

Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandwe akieleza hatua zilizofikiwa katika kuhakikisha kuwa watumishi wote wa Serikali wanahamia Dodoma wakiwemo wa Taasisi za Serikali na Mihimili yote.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Agustino Tendwa akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi. Maimuna Tarishi wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya Ofisi hiyo kutoka Jijini Dar es Salaam leo Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi. Maimuna Tarishi akikagua sehemu ya vifaa vya Ofisi hiyo vilivyowasili kutoka Jijini Dar es Salaam leo Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi la Serikali kuhamia Dodoma.

Sehemu ya vifaa vya Ofisi ya Waziri Mkuu vikishushwa katika moja ya magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali kuhamia Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi. Maimuna Tarishi akikagua sehemu ya vifaa vya Ofisi hiyo mara baada ya kufikishwa Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Bi. Maimuna Tarishi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ofisi hiyo na kikosi kazi cha kitaifa cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma leo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kupokea sehemu ya vifaa vya Ofisi ya Waziri mkuu iliyofanyika katika Ofisi hizo.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama